Donald Trump amechapisha tena picha ya wanawake wanane wa Iran wanaodaiwa kuwa katika hatari ya kunyongwa na kuwataka waachiliwe huru.
Kupitia mtandao wake wa Truth Social, aliandika: �Kwa viongozi wa Iran ambao hivi karibuni wataanza mazungumzo na wawakilishi wangu, nitashukuru sana kwa kuachiliwa huru wanawake hawa.�
Aliongeza: �Tafadhali msiwadhuru, na hili litakuwa mwanzo mzuri wa mazungumzo yetu.�
Mwishoni mwa Januari, kabla ya vita kuanza, rais huyo wa Marekani aliwashukuru viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kile alichokiita �kufutwa kwa hukumu za kunyongwa kwa zaidi ya watu 800.�
Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Iran amezitaja kauli hizo kuwa hazina msingi wowote.

Loading comments...